Kuhakikisha kuwa sera za matumizi ya fedha za serikali zinafuatwa kikamilifu kama zilivyo hainishwa kwenye mamlaka za serikali za mitaa na sera nyinginezo za matumizi ya fedha.
Kufanya ukaguzi wa matumizi ya ankra zote za halmashauri kila robo mwaka na kuandaa ripoti kwa afisa masuuli kabla ya tarehe 15 ya mwezi unaofuata robo husika.
Kufanya ukaguzi wa miradi na mali zote za halmashauri na kuhakiki uwepo wake kulingana na vitabu vinavyoonyesha (register) na kuandika taarifa na kuiwasilisha kwa afisa masuuli.
Kupitia na kuangalia utendaji na mfumo wa kila siku wa halmashauri na kuangalia kama utekelezaji.
Kupitia majibu ya hoja za ukaguzi zinazojibiwa na wakuu wa idara na kushauri njia sahihi ya kutatua kurekebisha changamoto zinazojitokeza.
Kuangalia na kukagua mifumo ya computer inayotumiwa na halmashauri na Kutoa ushauri kwa afisa masuuli juu ya ya ufanisi wake au matatizo yanayoikabali mifumo hiyo na namna ya kukabiliana na changamoto zake.