Kuratibu na kufuatilia kazi zote za mipango ya maendeleo katika halmashauri ya wilaya
Kuratibu mipango ya maendeleo inayofadhiliwa na serikali kuu na wahisani.
Kuchambua, kuthibiti na kuoanisha bajeti ya Serikali kwa kushirikiana na Wizara ya Fedha na TAMISEMI
Kutembelea miradi ya maendeleo iliyopo katika vijiji vinavyozunguka
Kuandaa taarifa za ilani ya uchaguzi zilizotekelezwa na idara za halmashauri
Kutafasiri sera na shughuli za halmashauri ya wilaya kwa wadau mbalimbali wa halmashauri ya wilaya
Kuhamasisha jamii kuanzisha biashara ndogondogo na viwanda vya uzalishaji
Kufanya mikutano ya kuhamasisha maendeleo kwa kushirikiana na NGOs,CBOs na FBOs zinazoshirikiana na halmashauri ya wilaya ya Nachingwea kwa kubadilishana uzoefu.
Kuratibu na kusimamia ushirikishwaji wa sekta binafsi katika shughuli za maendeleo
Kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo
Kufanya tathimini ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo
Kushirikiana na Idara zote kutoa mafunzo kwa watendaji wa kata na vijiji kuhusiana na mipango shirikishi ya maendeleo
Kutembelea asasi za kiserikali na zisizo za kiserikali kuona, kutoa ushauri wa kitaalamu na kutathimini mafanikio ya shughuli walizozifanya.
Kuratibu na kufuatilia kazi za mipango ya maendeleo katika halmashauri ya wilaya ya Nachingwea
Kuandaa maandiko mbalimbali ya miradi ya maendeleo kutokana na vipaumbele vinavyotolewa na wananchi
Kuandaa sera, mipango, mikakati na shughuli za halmashauri ya wilaya kwa wadau mbalimbali wa halmashauri ya wilaya.
Kutayarisha Mpango kazi wa mwaka.
Kukusanya taarifa mbalimbali za idadi ya watu, kuzichambua na kutafasiri kwa watendaji wengine wa H/W ya nachingwea
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.