Ni kuanzia Julai 29 mpama Julai 31 katika hospital ya wilaya ya nachingwea ambako kambi hiyo ya machona imetoa kutoa matibabu ya huduma za macho za kibingwa bure ambayo imefadhiliwa na Mo Dewji foundation kwa kushirikiana na Mkuu wa wilaya ya Nachingeea.
Mkuu wa Wilaya Mheshimiwa Mohamed Hassan Moyo amewapongeza wananchi wote wa Nachingwea kwa kuchangamkia fursa hiyo kwani matibabu hayo ni ya gharama sana lakini pia ametoa shukurani za dhati kwa uongozi wa Shirika la Mo Dewji Foundation kwa kukubali ombi lake na kuleta huduma Nachingwea.
Kwa upande wake Bi.Amina Ramadhan ambaye ni Program Coordinator wa Shirika la Mo Dewji Foundation na ndiye Mratibu Mkuu wa kambi hiyo macho ameeleza namna shirika hilo lilivyotoa huduma katika maeneo mbalimbali pamoja mpaka kufika wilaya ya Nachingwea, Madaktari bingwa 30 wa macho kwa kushirikiana na wataalamu wengine 20 kutoka Hospitali ya Nachingwea wameza kutibu wagonjwa zaidi ya 4900 kwa siku zote tatu.
Aidha, Katika ya idadi hiyo ya wagonjwa, 310 kati yao wamefanyiwa upasuaji, wagonjwa zaidi ya 2000 wamepatiwa miwani na wengine wamepatiwa dawa na kuanzishiwa kliniki, pia wananchi mbalimbali wameeleza maoni yao kuhusu huduma zilizotolewa katika ya kambi hiyo ya macho ambapo wengi wameonesha kufurahishwa na huduma hizo wameiomba Mo Dewji Foundation kurudi tena Nachingwea na kuendelea kuwapa huduma watanzania wengine.
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.