Watumishi watakiwa kufanya kazi kwa bidii na kujituma
Watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Nachingwea wametakiwa kufanya kazi kwa bidii na kujituma ili kutoa huduma bora kwa wananchi wanaowahudumia.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Hahim Komba, alipokuwa akiongea na watumishi na wakuu wa Idara na vitengo jana kwa nyakati tofauti.
Amewataka watumishi kufanya kazi kwa kujenga mahusiano yenye tija na kuheshimiana kwa lengo la kuijenga Halmashauri ya Nachingwea na watu wake.
“Tunatakiwa kujenga mahusiano bila kuathiri nidhamu katika Utumishi wa Umma, watumishi wanatakiwa kuheshimu mamlaka zilizopo miongoni mwetu kila mmoja aheshimu mamlaka ya mwenzake” Alisema Mheshimiwa Komba
Aidha, aliitka Halmashauri kuwashirikisha maafisa tarafa kwenye zoezi la kukusanya mapato ya Halmashauri katika maeneo yao ya kiutawala
Akiwa katika Viwanja vya Stendi ya zamani aliagiza taka zote zilizopo katika kizimba cha maeneo ya Stendi ziondolewe na eneo hilo kuwa safi kwa dhamira ya kuuweka mji katika hali ya usafi.
Pia, amewahimiza wananchi kushiriki katika kuuweka mji safi kwa kujitokeza kwa wingi katika zoezi la usafi la Jumamosi ya mwisho wa Mwezi kwa kila mmoja kwa kushiriki usafi katika maeneo yaliyopangwa na majumbani mwao.
Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya , Hashim Komba ameteuliwa hivi karibuni na Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli baada ya aliyekuwepo Rukia Muwango Kutenguliwa.
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.