Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya Nachingwea, Mhandisi Chionda M.Kawawa ametangaza rasmi ujio wa msimu wa pili wa Kituo cha huduma jumuishi maarufu kama ONE STOP CENTER,
Ameyasema hayo alipokua akizungumza na waandishi wa habari leo Agosti 29, 2025 katika ofisi ya Mkurugenzi,
Mhandisi Kawawa, ameeleza kwamba Tamasha hili ni mwendelezo wa Tamasha lililofanyika mwaka jana novemba 2024, ikiwa ni msimu wa kwanza na takribani wananchi 8600 walipata elimu na huduma kutoka katika ofisi na taasisi mbalimbali,
Pia ameongeza kuwa Kituo hiki cha huduma jumuishi huleta manufaa makubwa kwa wananchi na jamii kwani watu wote wanapata huduma mbalimbali katika eneo moja na huduma ambazo zinatolewa ni Afya na vipimo, elimu ya Lishe na mazingira, elimu ya fedha na huduma za kibenki, elimu ya ukatili wa kijinsia na watoto, upatikanaji wa vitambulisho vya nida na vyeti vya kuzaliwa, elimu ya mikopo ya serikali inayosimamiwa na idara ya Maendeleo ya jamii lakini pia fursa za kibiashara na kiuchumi,
Aidha Mkurugenzi amesema kwa mwaka huu, msimu wa pili wa Tamasha hilo unatarajiwa kufanyika Octoba 1 hadi 3,2025 katika viwanja vya maegesho ya malori na itakua ya tofauti kwani wamejipanga kutoa huduma nyingi na bora, pia kutakua na usafir kwa ajili ya kuleta na kuwarudisha watu kutoka sehemu mbalimbali ndani ya wilaya ya Nachingwea ili kuwafikia wananchi wengi zaidi, Tofauti na kutoa huduma kutakuwa na Bonanza la michezo likihusisha marathon na michezo mbalimbali katika siku ya ufunguzi.
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.