Mkuu wa divisheni ya Utawala na Utumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea, Kwa niaba ya Mkurugenzi, Bi Rachel Lububu, amewataka wanafunzi kushiriki kikamilifu katika kuhamasisha jamii juu ya umuhimu wa Elimu ya Watu Wazima na Elimu Nje ya Mfumo Rasmi,
Bi Lububu ameyasema hayo leo, Agosti 22, 2025, wakati wa maadhimisho ya Juma la Elimu ya Watu Wazima na Elimu Nje ya Mfumo Rasmi yaliofanyika katika viwanja vya shule ya sekondari Nachingwea day, Ameeleza kuwa elimu hiyo ni nyenzo muhimu ya kuwawezesha kujikomboa ki lookmaisha, sawa na elimu ya kawaida, kwani inasaidia kupunguza changamoto za ujinga, maradhi na umasikini ambapo Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, alitambulisha kama maadui watatu wa maendeleo,
Katika hatua za kuunga mkono juhudi za wanafunzi hao, Bi Lububu ameahidi kutoa kiasi cha shilingi milioni moja (1,000,000/=) kwa ajili ya kusaidia maandalizi ya safari yao kuelekea mashindano ya Young Scientist Tanzania, Shule ya Nachingwea Day ilishika nafasi ya pili kwenye mashindano hayo mwaka jana, hatua iliyowapa heshima kubwa katika wilaya ya Nachingwea.
Aidha kwa niaba ya Wanafunzi wa shule ya Sekondari Nachingwea day, Abilah Selemani ametoa shukurani za dhati kwa serikali kwa kuboresha matumizi ya mifumo ya kidigitali ya kufundishia na kufanya kua mfumo rafiki wa kujifunzia.
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.