Wizara ya Madini imeupongeza uongozi wa mkoa wa Lindi chini ya Mhe. Zainab Telack, kwa kuandaa Maonesho ya Madini ambayo yametoa fursa na elimu mbalimbali kwa washiriki wote waliotembelea maeneo ya maonesho.
Akizungumza wakati wa kufunga maonesho ya madini mkoa wa Lindi,Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ambaye alikuwa mgeni rasmi alisema serikali ya mkoa wa Lindi imefanya kazi kubwa ya ubunifu kuanda maonesho hayo yenye tija kwa mkoa wa Lindi na Tanzania nzima.
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.