Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Mheshimiwa Mohamed Hassan Moyo amewataka wenyeviti wa vitongoji wanaounda baraza la mamlaka ya miji mdogo ambao wanamaliza muda wao kuepuka vitendo vya rushwa na kusaidia wananchi, hayo ameyasema Agosti 15, 2024 alipokua akivunja baraza hilo.
Mhe. Moyo amewasisitiza wenyeviti hao kuendelea kusaidia jamii pale watakapohitajika na kuhimiza usafi wa mazingira katika maeneo wanamoishi, kwa wale watakaogombea tena nafsi hizo basi wajiepushe na vitendo vya rushwa.
Pia, amewataka watendaji wa Kata kwa kipindi ambacho watakaimishwa madaraka ya wenyeviti hao wasijifanye miungu watu na badala yake wahudumie wananchi mpaka pale wenyeviti wengine watakapopatikana.
Aidha, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Nachingwea Mhandisi Chionda A. Kawawa amewapongeza na kuwashukuru wenyeviti hao kwa kushirikiana vizuri na watumishi pamoja na Halmashauri kwa ujumla.
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.