Wazazi watakiwa kutimiza wajibu katika elimu
Kiongozi wa mbio za mwenge Charles Kabeho amewataka wananchi kutimiza wajibu wao kwa kuwapatia watoto wao mahitaji muhimu yatakayowezesha kusoma kwa bidii masomo yao
Ameyasema hayo wakati akitoa ujumbe wa Mbio za Mwenge wa Uhuru katika viwanja vya Shule ya Sekondari ya Misufini iliyopo kata ya Mpiruka tarafa ya Naipanga leo mara baada ya kufika wilaya ya Nachungwea akitokea wilaya ya Ruangwa
“Serikali inatoa elimu bila malipo kwa kuleta fedha za kugharimia elimu na kujenga miundombinu yake ikiwemo vyumba vya madarasa, maabara, mabwalo,mabweni nk lakini hiyo haiondoi wajibu wa mzazi kumhudumia mwanae, wazazi wanawajibu wa kununua sare, viatu na madaftari kwa watoto wao”.Alisema Kabeho
Amesisitiza kuwa wazazi wanaweza wakaona utaratibu wanaona unafaa katika kuhakikisha watoto wanapata chakula shuleni ili kupunguza changamoto za utoro mashuleni kwani utaratibu huo umefanikiwa katika mikoa ya Njombe na Kilimanjaro
Mwenge upo wilaya ya Nachingwea kukagua , kuweka jiwe la msingi na kuzindua miradi ya elimu, afya,kilimo maji na miundombinu ya barabara,kauli mbiu ya Mwenge wa uhuru mwaka 2018 ni "Elimu ni ufunguo wa maisha, wezeza sasa kwa manufaa ya Taifa letu"
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.