Tarehe 18 julai 2025 halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea imeendesha mafunzo ya Mfumo wa Anuani za Makazi kwa Watendaji wa Vijiji, yenye lengo la kuwawezesha kusimamia kwa ufanisi utekelezaji wa mfumo huo unaosaidia kuimarisha utambuzi wa maeneo na kaya kwa ajili ya mipango na utoaji wa huduma mbalimbali kwa wananchi.
Mafunzo haya yamefanyika katika ukumbi wa Halmashauri na kuendeshwa na Salim Ntilla, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA, ambaye ameeleza majukumu muhimu ya Watendaji katika utekelezaji wa mfumo huu.
Kupitia mafunzo hayo, Watendaji wameelekezwa namna ya kushughulikia na kupitisha barua za utambulisho kwa wanafunzi wanaoomba mikopo ya elimu ya juu, kuwatambua wamiliki wa kaya pamoja na wategemezi wao, kusajili kaya mpya, kuboresha taarifa za kaya zilizopo, na kuhakikisha kila kaya inakuwa na anuani sahihi ya makazi.
Mfumo huu ni msingi wa kuboresha utoaji wa huduma serikalini, mipango ya maendeleo, na usalama wa wananchi. Halmashauri ya Nachingwea inaendelea kujenga uwezo wa Watendaji wake ili kuh
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.