Wasimamizi wa uchaguzi mkuu wa rais, wabunge na madiwani katika jimbo la uchaguzi Nachingwea wameaswa kuhusu kutokushiriki katika vitendo vya rushwa, hayo yamesemwa na afisa wa TAKUKURU Bw. Mafuru Aloyce wakati wa mafunzo ya kusimamia uchaguzi yanayoendelea kutolewa na Tume Huru ya Taifa uchaguzi.

Mafunzo hayo yameendelea leo Oktoba 27,2025 katika Chuo cha Ualimu Nachingwea na katika kata ya Nambambo, akizungumza katika mafunzo hayo Bw. Mafuru alisisitiza wajibu wa kutenda haki ili kuondoa malumbano na migogoro isiyo na lazima, aidha pia aliongeza kusema makosa ya rushwa yanalingana na makosa ya uhujumu uchumi ambapo adhabu yake yaweza kufikia kifungo cha miaka 20 hadi 30.

Pamoja na hayo Bw.Mafuru alisisitiza kwa kurudia kauli mbiu ya TAKUKURU, “kuzuia rushwa ni jukumu langu na lako tutimize wajibu wetu”.
Akichangia katika kutoa maoni yake jinsi mafunzo hayo yalivyoendeshwa mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo Bi.Leyila Miraji kutoka katika kata ya Nambambo alisema, “ mafunzo ni mazuri wawezeshaji wanaelezea hoja vizuri na hasa kuhusu rushwa tumeelekezwa vizuri juu ya adhabu itakayotokana na rushwa.”
Aidha pia Bw.Joseph Nyerere na Bi. Abiba Hamadi walipongeza Tume Huru ya Taifa Uchaguzi kwa maandalizi mazuri ya mafunzo hayo.
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.