Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashuri ya Nachingwea Mhandisi Chionda M. Kawawa ameshirki katika kikao cha kamati ya lishe wilaya na kuagiza kuwa lishe iwe ajenda ya kudumu ya wilaya,kikao hicho kimefanyika leo Novemba 26, 2025 katika ukumbi wa Halmashauri ya Nachingwea.

Akitoa maagizo katika kikao hicho Mhandisi Chionda amezitaka baadhi ya idara kuhakikisha kuwa suala lishe linapewa kipaumbele katika shughuli zao.

Mhandisi Chionda alisisitiza, “kitengo cha lishe kiongeze nguvu katika utafitina suala la lishe liwe ajenda ya kudumu ya wilaya ya Nachingwea,watu wa maendeleo ya jamii, watu wa elimu, ustawi wa jamii n.k watu wa lishe nataka wawepo.”

Aidha Mhandisi Chionda ameitaka kamati ya lishe kuandaa shughuli zenye tija na matokeo kwa jamii, amesisitiza kuwe na shughuli zenye matokeo kwa watoto na wamama wajawazito.

Awali akiwasilisha taarifa ya kamati ya lishe afisa lishe Bi.Dahalile Zubery alisema kuwa fedha zote zilizoombwa kwa ajili ya utekezaji wa afua mbalimbali za lishe zililipwa na shughuli zimetekelezwa kwa ufanisi, lakini pia kumekuwa na changamoto ya watoto wanaozaliwa na uzito chini ya 2.5kg.
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.