Mkurugenzi Mtendaji wa Halamashauri ya Wilaya ya Nachingwea Mhandisi Chionda M. Kawawa pamoja na Kamati ya Wakuu wa Idara na Vitengo wahudhuria mafunzo ya CSR yaliyotolewa na Wataalamu kutoka Ofisi ya Madini Mkoa, mafunzo hayo yamefanyika Desemba 3, 2025 katika ukumbi wa Mikutano wa Shule ya Wasichana ya Nachingwea.

Mafunzo hayo yamefanyika ikiwa ni hatua ya kuijengea uwezo Halmashauri hiyo ambayo hivi karibuni inaingia katika uchumi wa Madini, Mhandisi Kawawa amewataka Wataalamu wa Halmashauri kwa kushirikiana na Ofisi ya Madini kuhakikisha Elimu hiyo inatolewa kwa jamii ili kuwajengea uwezo, Pia ameagiza ofisi ya madini waandaliwe ratiba ili waweze kutoa elimu kwa waheshimiwa Madiwani na kila mtaalamu atoe elimu kwa umma kulingana na eneo lake lake.

Kwa upande wake Mhandisi Dickson Joram kutoka Ofisi ya Madini Mkoa wa Lindi amesema "Tuko tayari kutoa Elimu hiyo kwa waheshimiwa Madiwani na serikali za vijiji ambako uchimbaji unafanyika na tuna mpango wa kutoa elimu kwenye shule za sekondari ili waweze kujengewa uwezo wa namna ambavyo wanaweza kusoma na kua wataalam wa madini".

Afisa Madini Mkoa wa Lindi Mhandisi Emmanuel Shija amemsihi Mkurugenzi na kamati ya CSR ya Halmashauri ni lazima kuwe ufuatiliaji wa karibu kwa pamoja, Halmashauri na Ofisi ya Madini ili kuhakikisha CSR inapatikana na wananchi waweze kunufaika na uwekezaji huo ili mambo yaweze kwenda vizuri.

CSR ni Corporate Social Responsibility, Maana yake ni uwajibikaji wa kampuni kwa jamii, yaani kampuni kufanya mambo ya kijamii kama kusaidia miradi, kulinda mazingira, kusaidia elimu, afya nje ya biashara yao ya kawaida
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.