Dkt. Nikson David kutoka Hospitali ya Rufaa ya Sokoine ametoa wito kwa wananchi wa Wilaya ya Nachingwea kujitokeza kwa wingi kupata huduma za uchunguzi na matibabu ya uoni hafifu yanayotolewa katika Hospitali ya Wilaya ya Nachingwea Kitengo cha Macho.

Huduma hizo zimeanza kutolewa leo, tarehe 24 Novemba 2025 na zitaendelea hadi tarehe 26 Novemba 2025.

Huduma hizi zinatolewa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi kwa kushirikiana na shirika la CBM, ikiwa ni jitihada za kuhakikisha wananchi wanapata huduma za afya ya macho kwa wakati na bila gharama yoyote.

Dkt. David amesisitiza kuwa huduma hizo ni bure, hivyo wananchi wote wanahimizwa kujitokeza ili kufanyiwa uchunguzi na kupata matibabu stahiki.
Huduma zinaanza saa mbili kamili asubuhi.
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.