Assistant Inspector Asha Mponda kutoka Dawati la Jinsia na Wtoto Kituo cha Poliosi cha Nachingwea amewashauri Maafisa wa Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa jamii kuhakikisha wanawatumia Mangaliba na Warombo wa jando na unyago ili kuwafundisha Watoto maadili mema. Hayo ameyasema Leo February 27, 2024 alipokua katika kikao cha kujadili mambo mbalimbali kiuhusu Program Jumuishi ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Mtoto kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Nachingwea.
Afande Asha amewashauri maafisa hao kuwatumia mangaliba na warombo katika kuhakikisha Watoto wanaokwenda jando wanapata maadili mema, kwani yapo baadhi ya maadili ambayo sio mazuri Watoto wanayapata kutoka jando na hawawezi kuyasema wala kuyaancha. Hivyo kama wakipewa maadili mema wakayashika itasidia kukuza maadili mema.
Aidha, Afande Asha amewasihi wadau mbalimbali waliohudhuria kikao hicho na wasiohudhuria kuhakikisha wanashirikiana katika wapa Watoto malezi, makuzi na maadili mema ili kutengeneza Tanzania ya baadae iliyobora.
#tupovizuri
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.