Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii bi Lilian Mwelupungwi wa Halmashauri ya wilaya ya Nachingwea ameongkoza zoezi la kuwajengea wanawake uwezo wa kushiriki uchaguzi katika nafasi mbalimbali kwenye maeneo yao yaliyoratibiwa na UN Women na Halmashauri ya wilaya ya Nachingwea. Zoezi hilo limefanyika May 30, 2024.
Zoezi hili ni Mradi wa uongozi na haki za kiuchumi kwa wanawake katika serikali za mitaa. Lengo ni kumuinua mwanamke kiuchumi na kuangalia vikwazo vinavyomfanya mwanamke asishiriki katika fursa za kimaendeleo. Mradi huu ni wa miaka minne kwa kata mbili za Nangowe na Mtua za wilaya a Nachingera.
Bi Mwelupungwi amesema wanawame wanawajengewa uwezo ili waweze kujitokeza kugombea nyazifa mbalimbali za uongozi katika maeneo vyao. Pia, Wanaangalia malezi na makuzi yao ,Mila na desturi pamoja na kuwawezesha kiuchumi. Bi Mweluungwi ameishukuru taasisi ya UN Women kwa kuleta mradi huu wa wanawake wanajitokeza na wanaona umuhimu wakugombea nyazifa mbalimbali ili waweze kushiriki katika maamuzi. Amewataka kuondoa hofu na kutokua nyuma.
Beatrice wiliam mratibu wa mradi amesema wameazimia kumpa mwanamke namna mbalimbali za kujiamini ili waweze kupata uongozi katika uchaguzi huu wa serikali za mitaa.
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.