Makamo mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Nachingwea ambae pia ni Diwani viti maalumu kata ya Mpiruka Mhe. Veronica Makotha amewataka wanawake kufanya kazi ili kuleta maendeleo kwenye familia zao na kuacha utegemezi kwa waume zao.
Mhe. Makotha ameyasema hayo leo May 10, 2023 alipokua kwenye Kikao cha Uanzishaji na Uhuishaji wa Jukwaa la Uwezeshaji wanawake kiuchumi katika ngazi ya wilaya.
Aidha, Mhe. Makotha ametumia jukwaa hilo kuhamasisha kila kikundi cha wanawake kilichochukua mkopo wa asilimia 10 wanarejesha ili kuwapa nafasi wanawake wengine kupata mikopo
#tupovizuri
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.