Wananchi watakiwa kutumia hati milki za kimila kupata mikopo
Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa na Utawala Mheshimiwa Jasson Rweikiza amewataka wananchi wa Kijiji cha Mbondo Wilaya ya Nachingwea kuzitumia hati milki za kimila walizopewa.
Ameyasema hayo jana kabla ya kukabidhi hati 100 za kimila ambapo amesema
zinzweza kutumika katika kupata mikopo kutoka benki mbalimbali hapa nchini na kuboresha maisha yao.
“Tumieni hati hizi vizuri kwani mali, zitawasaidia kupata mikopo kutoka benki mbalimbali zilizopo hapa nchini, hati hizi ni kitu kikubwa sana” Aliongeza Mheshimiwa Rweikiza.
Aidha Mheshimiwa Rweikiza amemuagiza Mkurugenzi wa Mkurabita Tanzania kuhakikisha jengo la Ofisi ya Mkurabita Kijiji cha Mbondo ujenzi wake unakamilika mwaka huu wa fedha kwa kuwa limechukua zaidi ya miaka kumi kukamilika.
Akiongea katika mkutano huo Mkurugenzi wa Mkurabita, amesema Serikali inataka wananchi wake kuondokana na umasikini kwa kuongea na benki kuzitambua hati milki hizo.
Kamati ya kudumu ya Utawala Bora na Serikali za Mitaa ipo kwenye ziara ya kukagua shughuli za maendeleo zilizo chini ya Kamati hiyo.
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.