Wananchi watakiwa kuchagua viongozi waadilifu
Wananchi wametakiwa kuchagua viongozi waadilifu na wenye uwezo wa kutatua kero na changamoto zao na wanaochukia rushwa ili kuwaletea maendeleo katika maeneo yao katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mheshimiwa Godfrey Zambi alipfanya ziara ya kikazi yenye lengo la kukagua miradi ya maendeleo na kusikiliza kero za wananchi katika kata za Kiegei, Mtua, Naipanga, Nachingwea, Lionja na Ruponda.mwanzoni mwa wiki
Amesema kiongozi ni mwalimu na mtu anayeonesha njia kwa kwa wengine hivyo anatakiwa kuwa mtu sahihi, hivyo wananchi wanatakiwa kuwa makini katika kufanya maamuzi sahihi.
“Unachagua kiongozi mlevi, hana hata nyumba ya kuishi, kila siku siku unasikia ameshikwa ugoni, anatukana hovyo, kwa mtu kama huyo unajifunza nini kutoka kwake” Aliongeza Mheshimiwa Zambi
Amewataka wananchi kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa na kufanya kampeni za kistaarabu na kuheshimiana kipindi cha kampeni kitakapofika na kuepuka vuvugu.
Amewataka kuacha lugha za matusi na vitendo vyote vinavyoashiria kuvunja amani , kwani wote watakaokiuka sheria watashughulikiwa na vyombo vya dola.
Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unatarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu ambapo wananchi watapata fursa ya kuchagua wenyeviti wa vijiji na vitongoji pamoja wajumbe wa Halmashauri za vijiji.
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.