Kaimu Murugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea ambae ni Afisa Mipango wa Halmashauri hiyo ndugu Joshua Mnyang'ali amewataka wananchi wa Kijiji cha Kiegei A kiichopo kata ya Kiegei kuunga mkono jitihada za Seeikali kwa kushiriki katika miradi ya maendeleo.
Mnyang'ali amewasihi wananchi hao kuwatumia wataalamu wa Halmashauri hasa Wahandisi katika miradi ya unenzi ili kupata taarifa na ushauri wa kitaalamu namna ya kutekeleza miradi hiyo.
Wananchi wa Kiegei A wametakiwa kuacha tabia ya kulumbana wakati wa utekelezaji wa miradi na badala yake kushiki kikamailifu katima miradi ya maendeleo, pia wamesisitizwa kushiriki katika mradi wa nyumba moja ya mwalimu uliyopo katika shule ya msingi Kiegei A wenye thamani ya shilingi milioni 51 ili kukamilisha kwa wakati ili walimu waweze kupata miundombinu bora ya kufundishia.
Aidha, Mnyang'ali amewapongeza wananchi hao kwa kua na nia madhubuti ya kutaka kukamilisha mradi huo kwa wakati na kuhakikisha kiasi cha fedha kinabaki na kuelekeza katika kutatua changamoto zingine katika shule hiyo.
Kwa upande wao wananchi wameishukuru Seeikali na Halmashauri kwa kupeleka mradi huo kwani shule hiyo inakabiliwa na changamoto ya miundo mbinu chakavu.
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.