Chama Kikuu cha Ushirika RUNALI kimefanikiwa kuongoza mnada wa tatu wa zao la korosho katika kijiji cha Tuungane, kata ya Maili Saba, Wilaya ya Liwale. Katika mnada huu, jumla ya kilo 14,516,790 zimepelekwa sokoni, ambapo bei ya juu Sh 3,390 na bei ya chini Sh 3,110.
Mwenyekiti wa chama hicho, Odasi Mpunga, amewashukuru wakulima kwa kujitokeza kwa wingi katika mnada huu wa kwanza kufanyika katika eneo hilo, huku akisisitiza juu ya uzalishaji wa kiwango cha juu.
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri, ndugu Haji Likoko, pia amepongeza uuzaji wa korosho kwa asilimia kubwa. Amehimiza wakulima kuhakikisha wanatoa korosho bora, akionya kwamba kupeleka korosho ghalani bila kukauka vizuri kunaweza kusababisha bei kushuka.
Tunawatia moyo wakulima wote kuendelea na juhudi hizi za uzalishaji na ubora ili kuinua thamani ya korosho zetu.
#Tupovizuri
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.