Mnada wa kwanza wa zao la mbaazi umefanyika katika kijiji cha Mkonjela kwenye chama cha Ndangalimbo Amcos, katika mnada huo wakulima wamekubali kuuza tani 6,255 kwa bei ya juu sh 1920 na bei ya chini 1870.
Katibu Tawala msaidizi wa Uchumi na Uzalishaji mkoa wa Lindi bwana Majid A. Myao amewasisitiza wakulima kupeleka mbaazi safi ili kuongeza thamani sokoni, pia amewataka msimu ujao kupanda mbegu bora za kisasa na kuchangamkia zao la choroko ili kuongeza mazao ya biashara kwenye mkoa wa Lindi.
Kwa upande wake ndugu Christopher Mkuchika akimwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea amewataka wakulima kuacha tabia ya kupeleka mazao wilaya jirani jambo ambalo linaipotezea mapato wilaya ya Nachingwea.
Wakulima nao wamefurahi kuuza kwa bei hizo na mfumo huu TMX umekua wa uwazi .wito wa kwa chama kikuu Runali malipo yawahi mapema
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.