Mnada wa tanowa zao la mbaazi umefanyika leo Agost 1, 2024 katika ofisi kuu ya Chama kikuu cha ushirika RUNALI ambapo wakulima wamekubali kuuza mbaazi zaidi ya tani 4500 kwa bei ya juu sh 1805 na ya chini 1760.
Ndugu Christopher Mkuchika ambae ni Afisa Tarafa ya Nambambo akimwakilisha Mkuu wa wilaya ya Nachingwea ameipongeza serikali ya awamu ya sita kwa kutafuta masoko ya zao la mbaazi na amekipongeza chama cha RUNALI kwa kazi kubwa wanayoifanya kwa wakulima, pia amewapongeza wataalamu wa TMX kwa ufanisi wao wa kazi.
Aidha, Meneja wa RUNALI Bi.Jahida Hassani amesema hadi kufikia mnada wa tano wamefanya malipo ya zaidi Shilingi bilion 26 kwa wakulima wa zao la mbaazi huku matarajio ya ukusanyaji wa zao hilo yanatarajia kuwa zaidi ya msimu uliopita ambapo runali ilikusanya tani elfu 17 ikiwa hadi sasa imekusanya tani elfu 20 hadi kufikia mnada huu wa tano huku makadirio yakiwa ni kukusanya tani elfu 22.
#Tupovizuri
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.