Mganga Mkuu wa Hospitali ya Nachingwea Dr. Ramadhani Mahiga amewataka wasimamizi wa Vituo vya Afya na Zahanati kuzibgatia maadili na taratibu za kazi zao na kutojiingiza katika vitendo visivyofaa kama kuwatoza fedha wamama wajawazito kwa ajili ya kuchangia huduma katika vituo vyao vya kazi. Dokta Mahiga ametoa kauli hiyo katika zahanati ya kiijiji cha Naipingo wakati akifanya ziara ya kukagua ujenzi wa zahanati na vituo vya afya.
Katika ziara hiyo iliyofanywa na Mkuu wa Idara ya Mipango na Uratibu kwa akimwakilisha Mkurugenzi Mtendaji Ndugu Joshua Mnyang'ali, Dr.Mahige alipokea maswali kutoka kwa Wanachi ya kutaka uelewa wa masuala mbalimbali kihisi huduma za Afya, katia ziara hiyo pia walikagua ujenzi wa zahanati ya Naipingo ambayo ujenzi wake umekamilika kwa kiasi kikubwa.
Wananchi wa kijiji cha Naipingo waliomba Zahanati yao ikamilishwe kwa haraka na kuanza kutoa huduma ili kuepuka changamoto wanazopata za kutembea umbali mrefu kufuata huduma katika zahanati ya Kihuwe, Dr.Mahige alifanya mawasiliano na Mganga Mfawidhi wa zahanati ya Kihuwe na kumtaka kuimarisha utolewaji huduma na kuzingatia maadili na taratibu za kazi zao.
Ndugu Rose Benedicto Milanzi na Fatuma Matuta wakaazi wa kijiji cha Naipingo kwa pamoja waliomba Zahanati yaNaipingo kikamilishwe haraka ili kupunguza adha wanazokumbana nazo katika kutafuta huduma za Afya.
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.