Shirika lisilo la kiserikali la Tanzania Forest Conservation Group (TFCG), kwa kushirikiana na MJUMITA(Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu Tanzania), Chuo Kikuu cha Leeds (LEEDS University) na CLIM-EAT, limeamua kupaza sauti kwa Serikali kuhusu mahitaji ya wakulima wa maeneo ya Kilimarondo, Namatula na Kiegei, hususan katika upatikanaji wa ruzuku kwa ajili ya kilimo chenye tija na endelevu.
Shirika hilo limeeleza kuwa dhamira yake ni kuwawezesha wakulima na wafugaji pamoja na kulinda mazingira, Katika juhudi zake za kuwashauri wakulima juu ya mbinu bora za kilimo cha mavundu, wamebaini kuwa changamoto kubwa inayowakabili ni upatikanaji wa pembejeo kwa wakati unaofaa.
Wakulima hao wamesema kuwa kwa sasa wakala wa pembejeo yupo umbali mkubwa, hali inayosababisha gharama za ziada na hivyo kushindwa kupata pembejeo kwa wakati sahihi wa msimu wa kilimo.
Akizungumza katika shughuli hiyo Meneja Mradi wa Mavundu kutoka TFCG Bi.Nuru Nguya amesema kuwa ili kuendeleza uhifadhi wa mazingira, wakulima na wafugaji wanapaswa kupewa maeneo maalum ya kudumu kwa ajili ya kilimo badala ya kuhamahama kutafuta rutuba katika maeneo mbalimbali.
Ameongeza kuwa suluhisho la changamoto hiyo ni kusogeza huduma za pembejeo karibu na wakulima, jambo litakalosaidia kuongeza tija ya uzalishaji na kulinda mazingira.
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.