Chama kikuu cha ushirika RUNALI kinachohudumia Wilaya tatu Ruangwa Nachingwea na Liwale kimeongoza mnada wa sita wa zao la mbaazi katika ofisi za chama hicho wilayani Ruangwa leo Septemba 4 2024 huku zaidi ya tani laki nane zimepelekwa sokoni ambapo bei ya juu ikiwa ni sh 1760 na bei chini ni sh.1730
Akizungumza na wakulima Mkaguzi wa ndani wa Chama hicho ndugu John Mwakipesile amesema kuwa kupanda na kushuka kwa bei za minada ya mbaazi ni kutokana na mahitaji ya wanunuzi sokoni kwa wakati husika kwani mfumo wa manunuzi wa sasa unakutanisha wanunuzi wengi katika mnada wa siku husika lakini pia kupanda na kushuka kwa bei hizo kunategemea bei iliyopo katika soko la dunia kwa wakati huo
Aidha, kwa upande wake Mheshimiwa Mohamedi Likoko ambae ni Makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Liwale amewataka wakulima kuhakikisha wanaandaa mazao yao katika ubora na usafi ili kukwepa panda shuka za bei ya mazao.
Nao wananchi wamekubali kuuza mbaazi kwa bei hiyo huku wakiiomba serikali kuboresha bei pamoja na kupunguza makato.
#Tupovizuri
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.