Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Mheshimiwa Mohammed Hassan Moyo ameshiriki kama mgeni rasmi katika sherehe za kuhitimu mafunzo ya JKT kwa mujibu wa sheria zilizofanyika leo Septemba 9, 2024 katika viwanja vya JKT kwa vijana wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na miaka 60 ya jeshi hilo.
Awali akitoa salamu za pongezi kwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe Dk SAMIA SULUHU HASANI kwa kuendeleza mafunzo hayo ya vijana amewataka kuwa wazalendo pia ameeleza kuwa matunda ya kazi hiyo ni kuwa na walinzi wa taifa na wazalendo na kuwataka vijana hao kuto rubuniwa na mtu yeyote na kujiunga na vikundi vya kighaidi.
Katika hatua nyingine Mhe Moyo ameeleza kuwa Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mhe Dk SAMIA SULUHU HASSAN tayari ameshatenga fedha zaidi ya bil (59) kwa ajili ya ukarabati wa barabara itokayo JKT mpaka mapochelo sambamba na upatikanaji wa mawasiliano ya simu katika eneo hilo na maeneo ya jirani.
Akisoma taarifa fupi Luteni Kanali Nyagaru Malecela ambae ni kamanda kikosi namba 843JK amesema kuwa vijana hao walianza kupokelewa mnamo june 1 na kufunguliwa june 19 na kufungwa sep 9 hivyo hivyo mafunzo hayo yamechukua takribani miez mitatu (3) na vijana 5 walishundwa kuendelea kwa sababu mbalimbali.
Nae kanali Barongo Kazaula muwakilishi wa mkuu JKT amewapongeza vijana hao kwani wamejifunza vitu mbalimbali ikiwemo vya darasani na uwanjani hivyo serikali inatambua na kuthamini uwepo wa JKT na kuwataka kuwa mabarozi wazuri kwa kuelimisha jamii kujiunga na mafunzo ya jeshi hilo.
Brigedia Generali Christina Shushi amewaasa vijana hao kupenda kazi yao kwa moyo na kuwataka vijana hao kukumbuka kuwa vijana ni taifa la leo na kesho akamaliza kwa kuwapongeza kwa kujiunga na kuhitimu mafunzo hayo.
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.