Wachimbaji wadogo Nditi wahakikishiwa kupata eneo la uchimbaji
Waziri wa Madini, Dotto Biteko amewahakikishia wachimbaji wadogo wa madini wa Kijiji cha Nditi kuwa watapata maeneo ya kufanyia kazi mara baada ya taratibu kukamilika
Waziri Biteko ameyasema hayo jana katika kijiji cha Nditi wakati akiongea na wachimbaji wadogo na wanakijiji katika mkutano wa hadhara uliofanyika kijijini hapo
Amesema kuwa Kampuni ya Ngwena ilipewa leseni ya kufanya utafiti wa madini ya nikel na Kopa ambapo kwa sasa leseni hiyo imesitishwa, mara baada ya maamuzi ya Baraza la mawaziri wachimbaji wadogo watapewa eneo la kuchimba madini.
Amewataka wananchi wa maeneo hayo na wachimbaji kuwa watulivu wakati wakisubiri maamuzi ya serikali
”Utaratibu wa kukuta wananchi wanachimba madini na kuwaondoa ni zilipendwa katika Serikali hii ya awamu ya tano, kama hawana leseni kazi ya Serikali hii ni kuwaelekeza na kuwasaidia wapate leseni” Alisema Waziri Biteko.
Aidha, Mbunge wa Jimbo la Nachingwea MheshimiwaHassan Masala amesema wananchi wanataka kujua hatma ya kampuni ya Ngwena kufanya utafiti katika kijiji hicho kwani utafiti wao umechukua muda mrefu.
“Mheshimiwa Waziri wananchi hawa wanataka kujua hatma ya utafiti wa madini unaofanyika hapa Nditi, Kijiji na Wilaya kwa ujumla wamenufaika vipi na utafiti huu kwa ujumla.
Waziri Dotto Biteko amefanya ziara ya kikazi ya siku moja Wilayani Nachingwea kufuatia mwaliko wa Mbunge wa Jimbo la Nachingwea Mheshimiwa Hassan Elias Masala.
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.