Chama kikuu cha ushirika Runali kimekabidhi printer 106 kwa vyama vya msingi katika Wilaya za Liwale, Ruagwa na Nachingwea zenye thamani ya zaidi ya shiling mil 80.
Akikabidhi vifaa hivyo mgeni rasmi Mkuu wa Idara ya Kilimo na Mifugo Bwana Raphael Ajetu amesema kuwa vifaa hvyo vitapunguza gharama ya matumizi ya fedha ya nauli kwa kwa wale wanaoishi maeneo ya pembezoni na mjini pia zitasaifdia katika urekebishaji wa makosa madogo madogo katika taarifa za mkulima pamoja na utoaji wa taarifa za mkulima kwa haraka.
Meneja Mkuu wa Chama hicho Bi.Jahida Hassani amesema kuwa printer hizo ambazo zimegawiwa kwa vyama 106 ndani ya wilaya hizo tatu lengo ni kurahisisha kazi kwa wafanyakazi na wakulima na kupata fedha za Malipo kwa wakati wafanyakazi wake walishapatiwa mafunzo kabla ya kukabidhiwa na zitakwenda kutatua changamoto ya umeme kwa kununua jenereta kwa baadhi ya maeneo (vijiji) ambayo wanachangamo hiyo.
Kwa niaba ya wapokeaji wa vifaa hivyo Bw Stephano Magavila ambae ni Katibu wa Nache Amcos ilyopo katika kijiji cha chemchem Amekishukuru chama hicho kwa kuwapunguzia changamoto ya kurudi stationary kurekebisha baadhi ya makosa madogo madogo kama vile majina ya wakulima kwaajili ya Malipo pamoja na uwandaaji wa taarifa kwa wakati nae Bi Awatu Mikolola ambae ni Katibu mkuu wa chama cha msingi Ndangalimbo ameongeza kwa kupongeza uongozi wa Runali kwani vifaa hivyo vitafanya mambo yaende kwa wakati na kuwaomba wafuatilie suala la umeme
#tupovzuri
@wizara_ya_kilimo
@bashehussein
@gm_runaliltd
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.