Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea kupitia Idara ya Maendeleo ya Jamii, imeendesha mafunzo kwa vikundi 55 vya wajasiriamali vilivyonufaika na mikopo ya asiliimia 10 ya mapato ya ndani, mafunzo hayo yamelenga kuwajengea uwezo kuhusu namna bora ya kusimamia na kurejesha mikopo hiyo.
Akizungumza wakati wa mafunzo hayo, Mwanasheria wa Halmashauri Bi. Diana Mmary, amesema kumekuwa na changamoto ya urejeshwaji hafifu wa mikopo, jambo ambalo linahusishwa na uelewa mdogo wa kisheria miongoni mwa wanavikundi.
Kwa upande wake Afisa Manunuzi Bi Adati Kana amezungumza kuhusu mambo ya kuzingatia katika kufanya manunuzi ikiwa ni kuhakikisha kabla ya kununua bidhaa kunafanyika malinganisho ya bei kutoka katika vyanzo vitatu tofauti na kuchagua bei ambayo ni rafiki kutokana na vyanzo hvyo, Pia kuwepo na Risiti halali ya bidhaa ni Muhimu katika kila file la kikundi.
Aidha, Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii ndugu Stella Kategile amewapongeza wajasiriamali hao na kuwasihi kuzingatia malengo ya fedha walizoomba kwa kufanya miradi waliyoiandika katika maombi yao, pia ameeleza kua kwa awamu hii ya pili shillingi millioni 649 zimekopeshwa kwa wanufaika hao.
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.