Kampuni ya Village Climate Solution Limited imeingia makubalino na Vijiji 16 vya Halmashauri ya Nachingwea kwa kusaini Mkataba wa Miaka 40 kwa ajili kufanya biashara ya Carbon ambayo hufaamika kwa jina la hewa ukaa, Mikataba hiyo imesainiwa Oktoba 18, 2024 katika ukumbi wa Halmashauri ya Nachingwea.
Mikataba hiyo imesainiwa mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Mheshimiwa Mohamed Hassan Moyo, Mwenyekiti wa Halmashauri Mheshimiwa Adnan Mpyagila, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ndugu Joshua Mnyang'ali na timu ya wakuu wa idara na vitengo wa Halmashauri hiyo.
Mhe. Moyo amewataka viongozi wa vijiji hivyo kuhakikisha sasa wanatunza misitu yao kwa nguvu zao zote kwani itakwenda kuwaletea tija katika biashara hiyo ambayo inategemewa kuanza kuwalipa hivi karibuni kabla ya mwaka wa fedha 2024/2025 haujamalizika, pia amewasihi kutunza misitu yao na kudhiti uvamizi na kuzuia migogoro isiyo na sababu ambayo inaweza kupelekea biashara hiyo kushindwa kufanyika vizuri.
Kwa upande wake mwakilishi wa kampuni ya Village Climate Solution Limited ndugu Emmanuel Kajumba ametoa pongezi kwa vijiji hivyo kuingia katika biashara hiyo kwani watakwenda kunufaika kwa kiaso kikubwa na kubadilisha maisha ya wananchi wao, kama kampuni jukumu lao ni kuhakikisha wateja wao wananufaika kwa maslahi ya nchi, tayari wanafanya biashara na Halmashauri 6.
Aidha Kaimu Mkurugenzi Ndugu Mnyang'ali amewataka watendaji wa vijiji hivyo kusimamia mradi huo kwa weledi wa hali ya juu na kwa kuzingatia utaratibu na mkataba waliosaini, pia kama kuna changamoto wataiona basi wafike ofisi ya Mkurugenzi kwa ajili ya kujadiliana.
Vijijj hivyo ni Kilimarondo, Mbondo, Ngunichile, Majonanga, Kiegei B, Kiegei A, Namatunu, Majengo, Nanjihi, Chimbendenga, Nakalonji, Lipuyu, Lionja, Mtua, Nahimba na Matekwe.
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.