Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea, Bi. Stella Kategile, ambaye ni Mgeni rasmi katika mkutano wakujadili Maendeleo ya mradi wa kituo cha Afya cha chiola na Maendeleo ya kata hiyo, amewataka wananchi wa eneo hilo kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa mradi huo,
Hayo ameyasema Agosti 19,2025 alipokua akiongea na wananchi katika mkutano huo, wakati wa ukaguzi wa mradi huo wenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 682, Bi. Kategile amewapongeza viongozi wa Vijiji na kata kwa ushirikiano wanaoendea kuonyesha katika kutekeleza mradi huo, Pia amewahimiza vijana wa Chiola kushiriki ili kuhakikisha ujenzi wa kituo hicho unakamilika kwa wakati uliopangwa.
Kwa upande wake, Mlezi wa Kata ya Chiola ambaye pia ni Mkuu wa kitengo cha mawasiliano Serikalini Halmashauri ya Nachingwea ndugu Faraja Raskombe, amewasihi wananchi wa kata hiyo kuuthamini mradi huo muhimu unaotarajiwa kuleta manufaa makubwa kwao na kwa vizazi vijavyo,pia amesisitiza umuhimu wa wananchi kushiriki na kufuatilia hatua zote za ujenzi ili kuhakikisha kituo cha afya kinajengwa kwa viwango vilivyopangwa na kwa matumizi ya muda mrefu.
Aidha kwa upande wao wananchi wameonyesha kuelewa na kuahidi kwa viongozi wa vijiji na kata kushiriki kikamilifu ili kuhakikisha mradi huo unakamilika na kuweza kupata huduma kwani wamekua wakilazimika kusafir umbali mrefu kufuata huduma za afya katika katabya marambo, pia wameishukuru serikali ya awamu ya sita chini ya Raisi Dkt. Samia Suluhu Hasani kwa kuendelea kuleta miradi ya maendeleo na yenye tija kwa jamii.
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.