Shirika ya Umoja wa mataifa la UNICEF limekabidhi kemikali za mabara kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea Mhandisi Chionda M. Kawawa zenye thamani ya zaidi ya Milioni 18 kwa ajili ya maabara za shule ya wasichana ya Nachingwea (Nachingwea Girls High School). Hayo yamefanyika leo Agosti 21, 2025.
Mhandisi Kawawa ametoa shukrani zake kwa UNICEF na Dokta Samila Suluhu Hassan kwa kuwezesha vifaa hivo kufika katika shule hiyo, pia amewataka walimu wa shule hiyo kuhakikisha vifaa hivyo vinatumika kwa ajili ya kuwafundishia wanafunzi na vitunzwe kwa uangalifu wa hali ya juu.
Aidha, kwa niaba ya idara ya Elimu sekondari Mkuu wa Divisheni ya Elimu Sekonadari Halmashauri ya Nachingwea Mwalimu Joas amemshukuru Mkurugenzi na shirika la UNICEF kwa msaada huo, kwani kulikua na uhaba wa vifaa na sasa vitakwenda kusaidia kwa kiasi kikubwa.
Ikumbukwe UNICEF ni shirika la Umoja wa Mataifa linalolinda na kukuza haki, afya na maendeleo ya watoto duniani
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.