Tarehe 26 Julai 2025 Taasisi ya kiraia ya FEMINA HIP (FEMA) imefanya bonanza kubwa la vijana katika Shule ya Sekondari Kipaumbele, likijumuisha shule kumi kutoka wilaya ya Nachingwea, mkoani Lindi, chini ya kauli mbiu “Vijana Wenye Maadili ni Msingi wa Maendeleo katika Jamii.”
Bonanza hilo limehusisha mashindano mbalimbali kama michezo ya kula, kucheza muziki (dance), uchezaji wa keyboard (DJ), kuimba na shindano la mavazi, likiwa na lengo la kuhamasisha mshikamano, maadili na usawa wa kijinsia kwa vijana.
Afisa Tarafa wa Nambambo, Ndugu Christopher Mkuchika, amemwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Mhe. Mohamed Moyo, ambaye alikuwa mgeni rasmi. Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya, Mkuchika amempongeza Mwenyekiti wa FEMA Kanda ya Kusini Mwl.Adam Matumbwa kwa kuandaa tamasha hilo akisema limeleta mshikamano, upendo na mahusiano bora kwa vijana.
Aidha, amewasisitiza wanafunzi kusoma kwa bidii kama njia ya kurudisha fadhila kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuwekeza kwenye miradi ya maendeleo, hususan sekta ya elimu katika wilaya ya Nachingwea.
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.