SHIRIKA lisilo la kiserikali la SWISSAID limeendelea kutoa elimu kwa wakulima kuendelea kulima kilimo hai ambacho ndio kitakuwa mkombozi kwa wakulima na wananchi wa Tanzania kwa kizazi cha sasa na kijacho kwa kuwa na afya bora.
Akizungumza Afisa miradi mwandamizi kutoka SWISSAID Bi. Veronica Masawe alisema kuwa lengo la shirika hilo ni kuhakikisha mbegu za asili zinaendelea kutumika kuzalisha mazao ya chakula kwa ajili ya chakula.
Masawe alisema kuwa mbegu za asili zimeanza kupotea hivyo jukumu lao ni kutoa elimu ya uhifadhi wa mbegu hizo na kuzizalisha kwa wingi ili ziweze kutumika nchi nzima na kuwawezesha wakulima kuacha kutumia mbegu za kisasa ambazo zinatumia madawa mengi ambayo sio nzuri kwa afya ya binadamu.
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.