Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa March 6, 2025 ameongoza kongamano la Wanawake kanada ya Kusini kuelekea maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika Wilayani Nachingwea Mkoani Lindi
Akifungua kongamano hilo, Mhe. Majaliwa amesema kuwa Serikali inatambua umuhimu wa kukuza usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa wanawake kama njia mojawapo ya kuimarisha ustawi na kufikia maendeleo jumuishi na endelevu.
Aidha, Waziri Mkuu amewataka wanawake kuendelea kuhamasishana na kutumia fursa zilizopo katika maeneo yao ikiwemo mikopo inayotokana na halmashauri (10%) na taasisi za kibenki kwa kuzingatia mikopo yenye masharti nafuu ili kutoathiri maendeleo na mienendo ya maendeleo ya mwanamke na mjasiriamali.
Kupitia kongamano hilo lililowakutanisha wanawake kutoka Mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma, wanawake wametakiwa kuanzisha viwanda vidogovidogo vya uchakataji ili kuongeza mnyororo wa thamani wa mazao ya kilimo wanayoyazalisha ili kujiongezea kipato
kupitia kuuza bidhaa badala ya malighafi. Mbunge wa Jimbo la Nachingwea Mhe Amandusi Chinguile ametoa shukrani zake kwa waandaaji wa kongamano na kuhitaji muendelezo wa matukio mengine ya kijamii, pia ameeleza baadhi ya mambo ya kimaendeleo yaliyotendeka katika wilaya hiyo ndani ya miaka 4 ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kama vile na uwepo wa vituo 6 vya afya, shule za msingi na sekondari ambazo zinaendelea kujengwa sambamba na ujenzi wa jengo jipya la Halmashauri linalogharimu zaidi ya Bil 4 lakini pia upandishwaji hadhi wa Hospital ya wilaya pamoja na ICU ya kisasa, upatikanaji wa pembejeo wa zao la korosho bila malipo upatikanaji wa mikopo kwa vikundi vya wanawake katika wilaya hiyo.
Naibu katibu mkuu wizara ya maendeleo ya jamii jinsia na makundi maalumu Bwana Amon Mpanju ameeleza kuwa wanawake wamekuwa ni muhimili na chachu kubwa ya maendeleo katika jamii hivo kuelekea siku ya wanawake ambayo itafanyika kitaifa katika mkoa wa Arusha huku Mhe Samia Suluh Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi, pia amewaomba wanawake nchini kujitokeza kwa wingi katika kugombea nafasi mbalimbali za uongozi
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.