Tarehe 28 Aprili 2025, Shirika la Sports Development Aid (SDA) kwa kushirikiana na Liike kutoka Finland, limetoa mafunzo ya huduma ya kwanza kwa Mangaliba na Walombo katika Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea. Mafunzo haya yamelenga kuwajengea uwezo washiriki katika kutoa huduma ya kwanza kwa majeruhi pindi ajali au madhara yanapojitokeza wakati wa shughuli za jando na unyago.
Akizungumza katika mafunzo hayo, Mratibu kutoka SDA, Ndugu Ramson Lucas, alisema: “Tunaamini kupitia ushirikiano wetu na Liike, tutaendelea kuwajengea uwezo viongozi wa mila ili kusaidia jamii kwa njia salama, bora na inayozingatia haki za watoto.”
Washiriki wameeleza kufurahishwa na mafunzo hayo wakisema kuwa yamewaongezea maarifa si tu kuhusu huduma ya kwanza, bali pia namna bora ya kuendeleza mila chanya na kuachana na mila potofu zisizofaa katika nyakati za sasa.
Mafunzo haya ni sehemu ya jitihada endelevu za kuimarisha afya, usalama na maendeleo ya kijamii kupitia urithi wa utamaduni unaobadilika kwa maslahi mapana ya jamii.
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.