Mnada wa tano wa zao la ufuta uliofanyika tarehe 13 Julai 2025 katika kijiji cha Luchelegwa, wilayani Ruangwa, umewezesha uuzaji wa kilo 3,825,910 kutoka maghala tisa ya wilaya za Ruangwa, Nachingwea na Liwale.
Chama Kikuu cha Ushirika RUNALI kimeuza ufuta kwa bei ya juu ya Tsh 2,560 na ya chini Tsh 2,530 kwa kilo.
Mwenyekiti wa RUNALI, Mh. Odas Mpunga, amewataka wakulima kuendelea kuzingatia ubora wa zao hilo ili kuongeza thamani sokoni. Afisa Masoko, Ndg. Emanuel Wilbert, amepongeza wakulima kwa uhifadhi mzuri na kuleta tija katika soko.
Wakulima wamekubali bei hizo na kupongeza usimamizi bora wa chama pamoja na utekelezaji wa maelekezo ya Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan.
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.