Tarehe 5 Aprili 2025, Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mheshimiwa Zainab Telack, amefanya ziara ya kukagua miradi mbalimbali itakayopitiwa na Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2025 katika Wilaya ya Nachingwea. Ziara hiyo ililenga kutathmini maendeleo ya miradi inayotarajiwa kukaguliwa na Mwenge wa Uhuru, na miradi aliyotembelea ni pamoja na ujenzi wa shule mpya katika Kata ya Chiumbati Milioni 560, mradi wa maji Naipanga bilioni 1.18 ,ujenzi wa kituo kidogo cha Polisi Naipanga Milioni 50, ujenzi wa zahanati ya Naipingo Milioni 56, na ujenzi wa barabara ya kiwango cha lami kutoka KKKT hadi Hospitali ya Wilaya (0.5 km) Milioni 356.
Pia, Mheshimiwa Telack amekagua kikundi cha vijana kinachotengeneza samani katika Kata ya Nachingwea Milioni 50 na mradi wa nishati safi ya kupikia katika Shule ya Wasichana Nachingwea Milioni 19, Katika ukaguzi huo, Mheshimiwa Telack ameeleza kuridhishwa na maendeleo ya utekelezaji wa miradi hiyo, lakini pia alitoa maagizo kwa wakandarasi kuhakikisha miradi ifikie asilimia 100 ya utekelezaji kabla ya ujio wa Mwenge wa Uhuru.
Akiwa katika ziara hiyo, Mheshimiwa. Telack amesisitiza umuhimu wa kuhakikisha kwamba utekelezaji wa miradi unahusisha matumizi bora ya fedha na kuzingatia muda wa utekelezaji. "Kasi ya ujenzi ni nzuri, lakini nataka kuona miradi yote imekamilika kwa viwango stahiki kabla ya ujio wa Mwenge," amesisitiza Mheshimiwa Telack.
Aidha, alitoa pongezi kwa Wilaya ya Nachingwea kwa kumaliza mradi wa nishati safi katika Shule ya Wasichana, amesema ni mfano mzuri wa miradi ya maendeleo inayozingatia mazingira na afya ya jamii.
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.