Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea Mhandisi Chionda M. Kawawa ameongoza wananchi na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea kufanya usafi katika eneo la Hospitali ya Wilaya ya Nachingwea na maeneo mbalimbali ya Mji wa Nachingwea.
Aizungumza na Wananchi na Watumishi mara baada ya kukamlika kwa zoezi hilo Mhandisi Chionda amewapongeza waliojitokeza na kuwasihi kuendelea kufanya usafi katika maeneo ya kijamii na katika makazi yao kwani kwa kufanya hivo pia inasaidi kufanya mazoezi ya mwili.
Aidha, amewapa motisha ya supu wakazi waliojitokeza katika kufanya usafi ili kuhamasisha na wengine kujitokeza, ikumbukwe hii ni katika kufanya usafi wa Mazingira ambao hufanyika kila Jumamosi ya Mwisho wa mwezi ambapo leo Septemba 27, 2025 ni jumamosi ya mwisho wa mwezi Septemba.
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.