Kwa kutumia mapato ya ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea, Milioni 20 zimetumika kuimarisha miundombinu ya upatikanaji wa maji katika Haospitali ya Wilaya ya Nachingwea kwa kuchimba kisima kitakachowezesha upatikanaji wa maji wa kudumu.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, ndugu Racheal Lububu Mkuu wa Idara ya Utawala na usimamizi wa Rasilimali watu amemesema lengo kubwa la Halamashauri ni kumaliza tatizo la maji na kuboresha miundombinu hiyo kwani kwa sasa katika kila jengo mabomba yatapelekwa na watumishi pamoja na wanachi watapata huduma za maji ya uhakika pia itasaidia katika ufanisi wa utolewaji wa huduma za matibabu.
Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa Hospitali, Dkt. Shukurani Msikini, amesema mchakato wa upatikanaji wa maji safi umekamilika kwa mafanikio makubwa, na hatua inayofuata ni kuhakikisha maji hayo yanasambazwa katika majengo yote ya hospitali na amesisitiza kuwa huduma hiyo itaboresha zaidi mazingira ya kazi kwa watumishi wa afya na kuongeza ufanisi katika utoaji huduma kwa wagonjwa.
Kwa upande wao wananchi wa Nachingwea wameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri, Mhandisi Chionda Kawawa, kwa jitihada za kuendelea kuboresha huduma za kijamii ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa maji hospitalini hapo kwani itapunguza changamoto zilizokuwa zikiwakuta na kuimarisha ustawi wa huduma kwa wananchi.
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.