Tarehe 2 mei 2025 Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mhe. Zainab Telack, amezindua rasmi Mpango Mkakati wa Elimu wa Mkoa wa Lindi kwa mwaka 2025, katika hafla iliyofanyika wilayani Ruangwa. Mpango huo unalenga kuongeza ufaulu na kuimarisha utoaji wa elimu bora kwa kushirikisha wadau wote wa elimu katika ufuatiliaji na utekelezaji.
Katika hotuba yake, Mhe. Telack amesisitiza usimamizi makini wa ufundishaji na ujifunzaji kwa kuzingatia miongozo ya elimu, mikataba ya utendaji kazi na maelekezo ya mpango huo. Pia amewapongeza walimu, wanafunzi na wasimamizi wa elimu kwa juhudi zilizowezesha mafanikio ya mkoa katika sekta ya elimu.
Aidha, amehimiza utoaji wa chakula mashuleni na kuimarishwa kwa elimu ya kujitegemea ili kuwajengea wanafunzi ujuzi wa maisha.
#Tupovizuri
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.