Agosti 15, 2024 imefanyika programu ya uwezeshaji wananchi Kiuchumi Mkoa wa Lindi iliyoambatana na mafunzo ya jinsi ya kujisajiri kwenye mfumo E-Dodoso liliofanyika kwenye ukumbi wa Kagwa mjini Lindi.
Bi.Beng'i Issa ambae ni Katibu Mtendaji wa baraza la taifa la uwezeshaji wananchi Kiuchumi amesema watachakata data za mkoa zilizoingizwa kwenye mfumo na wataleta vipaumbele ili na wao walinganishe na waliyoyasikia kutoka kwa wajasimali katika programu hiyo kwani wananchi wa lindi wanatamani program ianze ili wajikwamue kiuchumi.
Bi Beng'i ameutaka mkoa kuangalia vipaumbele na kuhakikisha programu zilizopo zinaendelea ili kuleta hamasa kama kilimo cha korosho kuongeza thamani ya mazao, Mwani na Uvuvi, kuhusu mikopo ya 10% amesema maelekezo yaliyotolewa na Serikali yafuatwe ili waweze kupata hiyo mikopo hiyo na waisimamie vizuri.
Aidha, ametoa wito kwa wananchi wa Mkoa wa Lindi ambao hawakuhidhuria programu hiyo waendelee kufanya kazi na waratibu waende kwenye ofisi za halmashauri ili waweze kuwasajili na zoezi la usajili ni wiki mbili.
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.