Leo tarehe 26 mwezi wa pili 2025 ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Nachingwea imekabidhi mifuko 91 ya saruji kwa Bi. Zuhura Mshana, aliyepoteza watoto wanne katika ajali ya moto iliyotokea Februari 15, 2025, mtaa wa Kalfania.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Nachingwea, Dkt. Ramadhani Mahige, alisema kuwa ofisi yake imeguswa na hali aliyo nayo Bi. Zuhura na kwamba msaada huu utawezesha kujenga nyumba mpya ili kuanzisha maisha mapya. Dkt. Mahige amesisitiza nimuhimu kuunga mkono familia hiyo katika kipindi cha majonzi.
Bi. Zuhura amemshukuru Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Nachingwea kwa msaada mkubwa aliopewa.
Aidha, mratibu wa zoezi hilo Ndg. Wakati Makona kutoka Kundi la WhatsApp la Nachingwea Yetu, amemshukuru Mkurugenzi kwa kuguswa kwake na saruji hii inaenda kusaidia ujenzi wa nyumba ya Bi.Zuhura na kuwaomba wadau kuendelea kuguswa ili kufanikisha ujenzi huo.
#Tupovizuri
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.