Tarehe fisi ya Maendeleo ya Jamii imefanya mkutano muhimu na wanafunzi wa shule za sekondari zilizopo katika Mamlaka ya Mji Mdogo wa Nachingwea, lengo likiwa ni kutoa elimu kuhusu masuala muhimu yanayohusu jamii, ikiwa ni pamoja na ukatili wa kijinsia, ushiriki wa vijana katika uchaguzi mkuu, na malezi bora ya watoto.
Mkutano huu umefanyika ikiwa ni maandalizi kuelekea Siku ya Wanawake Duniani, ambayo huadhimishwa kila mwaka tarehe 8 Machi. Kwa njia hii, ofisi imejizatiti kutoa ufahamu kwa vijana kuhusu umuhimu wa kujitokeza na kushiriki katika masuala ya kijamii na kisiasa, pamoja na kuelimisha juu ya madhara ya ukatili wa kijinsia na namna bora ya kulea watoto katika jamii.
Aidha, mafunzo haya yanatoa nafasi kwa wanafunzi kuwa na uelewa mpana kuhusu nafasi yao katika jamii na umuhimu wa kuchukua hatua katika kupambana na ukatili wa kijinsia na kuendeleza malezi bora ya familia.
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.