Katika siku ya Pili ya ziara yake mkoani Lindi, Mhe. Naibu Waziri OR-TAMISEMI, David Silinde ameipongeza Halmashauri ya wilaya Nachingwea kwa kujenga na kukamilisha madarasa yanayojengwa chini ya EP4R-T8 kwa ubora na viwango vinavyotakiwa.
Naibu Waziri ametoa pongezi hizo jana alipokuwa akikagua miradi ya ujenzi wa madarasa Shule ya Sekondari Nambambo na Nachingwea, ambapo ameridhishwa na ubora wa ujenzi wa madarasa hayo yanayotekelezwa chini EP4R-T8
“Madarasa yenye ubora wa namna hii yamezoeleka kuonekana katika Halmashauri za majiji na manispaa kubwa” Amesema Mheshimiwa Silinde hayo alipofika eneo la ujenzi kujionea shughuli za maandilizi ya ujenzi
Aidha, Mheshimiwa Silinde ameipongeza Halmashauri ya Nachingwea kwa uamuzi wa kujenga shule kubwa ya Wavulana itakayochukua zaidi ya wanafunzi 1500, ambapo kiasi cha shilingi Tshs.516,000,000/= zitokanazo na mapato ya ndani kimetengwa kutekeleza mradi huo.
Katika hatua nyingine, Naibu Waziri ameelekeza Halmashauri zote zenye mapato ya ndani chini ya 1.5 bilioni kutenga bajeti ya ujenzi wa madarasa 20 katika bajeti ya 2021/22, Kwa Halmashauri zenye mapato ya Tsh. 1.6 mpaka 5 bilion kutenga bajeti ya ujenzi wa madarasa 40 na zile zenye mapato ya zaidi ya Tsh. 5 Bil kutenga bajeti ya ujenzi wa madarasa 80.
Mheshimiwa Naibu Waziri yupo mkoani Lindi kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa.
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.