Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dkt. Edwin Mhede, jana tarehe 7 Agosti 2025, alitembelea banda la Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea katika Maonesho ya Nanenane Kanda ya Kusini yanayofanyika kwenye viwanja vya Ngongo mkoani Lindi.
Dkt. Mhede alipata fursa ya kukutana na wataalamu wa sekta ya kilimo, mifugo na uvuvi kutoka Halmashauri ya Nachingwea pamoja na wajasiriamali wanaoshiriki kuonyesha shughuli mbalimbali za uongezaji thamani kwenye mazao na huduma zao.
Akiwa kwenye banda hilo, Dkt. Mhede alionesha kuridhishwa na namna Halmashauri ya Nachingwea inavyoshirikisha jamii katika matumizi ya teknolojia na ubunifu katika kuendeleza uchumi wa kilimo na mifugo kwa vitendo.
Maonesho ya Nanenane Kanda ya Kusini ni jukwaa muhimu kwa wajasiriamali na wadau wa maendeleo ya kilimo kupata nafasi ya kujifunza, kujitangaza, na kupata masoko mapya kupitia Halmashauri zao.
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.