Mwenyekiti wa Halmashauri ya Nachingwea, Mheshimiwa Adinan Mpyagila, ameahidi kutoa shilingi laki tano katika hafla ya mahafali ya 15 ya shule hiyo,iliyombatana na harambee iliyofanyika jana tarehe 21/10/2024, katika shule ya sekondari kata ya Lionja. Pesa zilizokusanywa ni jumla ya shilingi 1,553,950, ambapo Mheshimiwa Mpygila ameahidi pia kutoa mpira, jezi, mafuta, unga wa wangano, na sukari kwa wanafunzi wa kidato cha nne ili kuwasaidia katika mtihani wao.
Katika hafla hiyo, Mheshimiwa Mpyagila alitoa vyeti kwa wanafunzi waliofanya vizuri na kuwatia moyo wanafunzi wote wa kidato cha nne. Aidha, alitangaza kuanza mara moja ujenzi wa choo cha walimu, ukikamilika kabla ya tarehe 30 Novemba.
Mwenyekiti alisisitiza umuhimu wa wazazi kuwa na matumizi mazuri ya fedha ili kusaidia maendeleo ya elimu ya watoto wao, na aliwapongeza walimu kwa ufaulu wa asilimia 100 katika matokeo ya kidato cha nne na na cha pili.
Pia, Mheshimiwa Mpyagila amezichukua changamoto za shule, ikiwemo ukosefu wa mwalimu wa kike, na aliahidi kuchukua hatua za haraka ili kutatua tatizo hili. Alifurahia juhudi za uandikishaji wa daftari la wakazi kwa uchaguzi wa serikali za mitaa, ambapo kata ya Lionja imefanikisha asilimia 107, ikiwa na zaidi ya watu 6000 waliojandikisha na kushika nafasi ya nane kiwilaya.
Aliwasihi wananchi kujitokeza kupiga kura na kuchukua fomu za kugombea nafasi mbalimbali za uongozi. Hii ni hatua muhimu katika kukuza elimu na ushiriki wa jamii katika maendeleo.
#Tupovizuri
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.