Mradi wa ujenzi wa Barabara ya Kanisa la KKT - Hospitali ya Wilaya wenye thamani ya Milioni 356 umewekewa jiwe la Msingi na kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2025 Ndugu Ismail Ali Ussi Mei 29, 2025.
Chanzo cha fedha za ujenzi wa mradi huu ni Tozo za Mafuta, barabara hiyo yenye urefu Kilomita 0.5 itakwenda kusaidia utolewa wa huduma kwa haraka hasa huduma za usafirishaji wa wagonjwa ukilinganisha na hapo awali ambapo wakati wa mvua barabara hiyo ilikua ni changamoto.
Aidha, kwa upande wake Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Nachingwea Mhandisi S.T. Kyamba amesema mradi huo ambao umeanza Septemba 20, 2024 unatarajiwa kukamilika Juni 17, 2025 .
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.