Mwenge wa uhuru unaendelea kutembelea miradi katika halmashauri ya Nachingwea ambapo umetembelea mradi wa vyumba vitano vya madara shule ya Msingi Nditi na kiongozi wa mbio za mwenge ndugu Godfrey Eliakim Mzava amerizika na mradi huo wenye thamani ya shilingi milioni 132
Ndugu Mzava amepongeza na kusisitiza kuwa ni vyema majengo yanayojengwa yawe yenye ubora na viwango kuendana na thamani aalisi ya fedha zinazotolewa Kwa ajili ya miradi husika.
Sambamba na hilo kiongozi huyo wa mbio za mwenge amezindua mradi wa usambazaji wa umeme vijijini (Rea) Pomoja na kutembelea katika mradi wa utunzaji wa mazingira miti katika kijiji cha Ruponda ambapo zaidi ya miti 600 imepandwa katika eneo hilo.
Aidha, ameeleza kuwa upandaji wa miti ni muhimu kwani inasaidia kupambana na mabadiliko ya tabia ya nchi.
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.